Koo Ya Msema Kweli: 'Msasi Haogopi Miiba'

Tembo aliyeuwawa























Tamko La Koo:
Msasi: Mtu anayewinda wanyama hasa kwa njia ya haramu.
Miiba: Namna ya majani yaliyopinda na kuwa mfano wa shindano lenye ncha kali.

Maelezo:

Huu msemo una maana kuwa mwindaji haramu akishaamua kuenda kushiriki mawindo ya namna isiyohalali, basi hana budi kutimiza malengo yake. Anakuwa ni mtu wa kujitolea ima fa ima bila woga.

Msemo huu unatumika kuwapa wosia watu wanaosuasua katika kutimiza malengo yao kwamba wasikate tamaa.

Ni jambo la bayana kwamba msemo huu una ukaribu na ule usemao mla ngurue humchagua aliyenona. 

Post a Comment

0 Comments