Koo Ya Msema Kweli: 'mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani'

wavuvi wakiwa katika mashua




























Misamiati katika msemo huu ni;

tezi; sehemu ya mbele ya mashua
omo; sehemu ya nyuma ya mashua
ngamani; sehemu ya kati ya mashua.

Huu msemo una maana kwamba popote uendapo, lolote ufanyalo, ni bora ukafahamu kwamba utarejea kule ulikotokea mara ya kwanza.

 Aghalabu msemo huu hutumika kuwakashifu watu wenye tabia ya kudhihaki maeneo waliotokea (chimbuko lao) ama jamma zao kwa ufanisi walionao.

Kwa hiyo, watu wenye tabia ya namna hii wanapata kuelewa kuwa wasikose heshima kwa watu au sehemu ambazo wamekulia maana huenda wakataraji kurudi sehemu zile ama kuwahitaji watu wale.

Msemo huu unakaribiana na msemo usemao usitupe mbachao kwa msala upitao.

Post a Comment

1 Comments