Huu msimu wa siasa, 
Chunga usije kuwaa kisiasa,
Ukauona mrefu na chungu,
Ukaja kuchana ukungu,
Zao tunu wenye haki!

Alilonga Joho,
Japo katu joponi,
Bali ya roho,
Kuwa kwema peponi,
Zao tunu wenye haki!

T'alonga hata lini,
Ee wanadamu vijiweni,
Baniani hawi mwema,
Japo salamu Kwema?
Zao tunu wenye haki!

Daima siasa mikiki,
Ee limbukeni ewe,
Uliyetayari mikiki,
Dua hino si la mwewe,
Zao tunu wenye haki!

Siasa kama falsafa,
Yahitaji asilani maafa,
Upevu akilini yatosha,
Ung'amuzi yamkini tosha!
Zao tunu wenye haki!

Kila la haki,
Msitilie huruma,
Wala imani dhihaki,
Imara kauli wima,
Zao tunu wenye haki!