SWAHILYRICS | UTANIPENDA LYRICS BY DIAMOND PLATINUMZ

By Sammy Anyona



Verse 1
Oh ghafla visenti sina nimerudi Tandale,
nimeshindwa kulipa bima, nimeuza madale,
redio nyimbo wamezima tv ndio hatare,
meneja umebaki jina, hanitakii ata Tale,
oh naye shabiki zangu walonisifu kwa maneno matamu,
leo madui zangu, ni mitusi tu kwa instagramu,
ee mwanastaa tangu, ati naye hanifahamu,
hata Harmonize, nikimpigia ananifokea kama salamu,
na magazeti nyumbani kwa kukuza habari, si unajuaga,
utasikia tafarani ati mondi kwa Zari amemwagwa,
na veye nilivyo mnyonge tabia ya kuwajibu sinaga,
kama naiona michango wa mademu wa zamani nlowapitiaga.

VERSE 2
Oh ninayosema yana maana
sababu hakuna anayejua kesho
anayepanga ni Rabana
ila ameficha ni confidential
ukisali omba sana
mumeo nisije kuwa kichekesho
maana rafiki wa jana
ndio adui mkubwa kesho…

(Chorus)
Oh Je utanipendaga
la la la la la la la
au nawe utanimwaga
la la la la la la la
ati utanipendaga

Verse 3
Oooh bado nawaza sana
zile tuzo umeshahudhuria pote
je ntapofika tama
utadirika hata japo kuniposti
pindi show zimekwama
na nikipata sijazi ni mikosi
oh jahazi limezama
Mola ninusuru Baba

Verse 4
Kama namwona mwanangu roho yangu,
Tiffah Dangote, anakwenda na mamangu,
kwa Jakaya Kikwete wanafukuzwa watoke,
uusilie sana mamangu, mwanangu,
jikaze usichoke huenda kesho zamu yangu nitavuma tena mambo yanyooke,
na magazeti nyumbani kwa kukuza habari si unajuaga,
utasikia tafarani ati mondi kwa zari amemwagwa,
na venye nilivyo mnyonge tabia ya kuwajibu sinaga,
kama naiona michango wa mademu wa zamani nlowapitiaga (…)
la la la la la la la
la la la la la la la
la la la la la la la

Verse 5
Kama namwona mwanangu roho yangu,
Tiffah Dangote, anakwenda na mamangu,
kwa Mkubwa Fella anafukuzwa atoke,
uusilie sana mamangu, maoni yangu,
jikaze usichoke huenda kesho zamu yangu,
nitavuma tena mambo yanyooke

Verse 6
Oh ninayosema yana maana
sababu hakuna anayejua kesho
anayepanga ni Rabana
ila Ameficha ni confidential
ukisali omba sana
mumeo nisije kuwa kichekesho
maana rafiki wa jana
ndio adui mkubwa kesho.


Mtunzi na mwandishi wa wimbo; Diamond Platinumz.

#Twitter @sammyanyona.
Feel free to comment... .

Post a Comment

0 Comments