Mkuu wamuziki wa aina ya ‘Genge’ uliovuma na kupasua anga sana nchini Kenya enzi za kale kidogo Prezzo, alitupasulia mbarika kwenye mahojiano ya televisheni ya KTN ya Kenya, taavgrifa za #FridayBriefing kuwa azma yake kuu anayolenga kutimiza maishani ni kuwa daktari.
Staa huyu ambaye alivumisha muziki wake na kuwa wa kimataifa alisema haya katika mahojiano na Betty Kyalo Okari alipoulizwa kuhusu azimio lake…
‘ Baba yangu alifungua Makini Herbal Clinic na mimi ni mtoto wa pekee wa kiume nyumbani, imenibidi nisome kuhusu masuala ya utabibu ili nisimamie shughuli za clinic… nitakuwa natoa huduma kwa watu na majaaliwa nitaitwa Dr. Jackson Makini. Nahitaji kuendeleza urithi wa kitu kizuri alichokijenga baba yangu’- Prezzo.
Alizidi kusema kuwa…
‘Namkumbuka sana mzee wangu, angekuwa hai najua angejisikia fahari kuwa na mtoto kama mimi… nadhani angekuwa hata Rais wa Kenya’ – Prezzo.
Wazo hili huenda ndilo lililompelekea kuadimika jina, kwa kiasi, kwenye muziki kulingana na mashabiki wake.
1 Comments
Hongera Sammy!!! Nimeipenda blog
ReplyDelete