Huu msimu wa siasa,
Chunga usije kuwaa kisiasa,
Ukauona mrefu na chungu,
Ukaja kuchana ukungu,
Zao tunu wenye haki!
Alilonga Joho,
Japo katu joponi,
Bali ya roho,
Kuwa kwema peponi,
Zao tunu wenye haki!
T'alonga hata lini,
Ee wanadamu vijiweni,
Baniani hawi mwema,
Japo salamu Kwema?
Zao tunu wenye haki!
Daima siasa mikiki,
Ee limbukeni ewe,
Uliyetayari mikiki,
Dua hino si la mwewe,
Zao tunu wenye haki!
Siasa kama falsafa,
Yahitaji asilani maafa,
Upevu akilini yatosha,
Ung'amuzi yamkini tosha!
Zao tunu wenye haki!
Kila la haki,
Msitilie huruma,
Wala imani dhihaki,
Imara kauli wima,
Zao tunu wenye haki!
17 Comments
Heko kwako kaka,,,, nafurahia wandishi wako haswa weledi upande was siasa,,, take it a notch higher for u can
ReplyDeleteAsante kwa mchango wako
DeleteKazi nzuri Sana Sam....endelea vivyo hivguo
ReplyDeleteAsante Anne
DeleteHeko kaka kazi nzuri sana!! Endelea vivyo hivyow
ReplyDeleteJames siasa ya 2017 ni kawaida wala si kufa kupona
DeleteBeen impartial n stating facts ..I like it.
ReplyDeleteThank you very much Jimmie
DeleteTouché my brother. Great command of language.sheria za ushairi nazo umezifuata kwa kina Na umakini. Hongera!
ReplyDeleteAsante, nashukuru. Mwana habembelezwi kwa wimbo mbaya, lazima uwe umekamilika.... Nakshi kidogo pia
DeleteKila ubeti una taarifa kikamilifu. Takhmisa nzuri kabisa. Heko!
ReplyDeleteAsante, ujumbe muhimu lazima utendewe haki, matayarisho yake, sheria halikadhalika
DeleteHongera ndungu yangu...kazi nzuri sana ...endelea kutia bidii
ReplyDeleteAsante dogo, mambo muhimu haya
DeleteKazi nzuri kaka. Zidi kupasa sauti haswa kuhusu siasa nasi tupamoja nawe
ReplyDeleteAsante sana
DeleteNimelipenda shairi
ReplyDelete