Lyrics to VifuuTundu by AT

Taarab singer AT


(wao)*4 wajuaju wa kusema (vifuu tundu)
(wao)*4 wanasema yasomanaa (vijitu)
ndo maana hawapokewi kwasababu wana laana
(hapo saae, hapa ndo kucha)*4

hodi hodi naingia, nazirejeesha salamu
mlango walopitia kupita mimi haramu
najua mna hamuu ugomvi kwenu tunu
mwenye akili timamu kugombana kwake sumu
(Maneno yenu wala hayafanyi mtu kuwa mwembamba, ndo kwanza azidi kunawiri kama shina la mgomba) {sauti}

 mna (pita)*3 kusema wasoyajua
[mna (zuwza)*3 mwishoni mtazomewa ]*2

(wao)*4 wajuaju wa kusema (vifuu tundu)
(wao)*4 wanasema yasomanaa (vijitu)
ndo maana hawapokewi kwasababu wana laana
(hapo saae, hapa ndo kucha)*4

 ujumbe ulinambia nkabisha katu katu
[katika hii dunia wengine majini watu ]*2
(mwanaamke mbeya utamjua tu mdomo wake, mweusii kama kunguru) {sauti}

 ninaona bora mfanye yanowahusu
[kuombea wenu msokiitwa kama kasuku]*2
mimi kama kasuku mnanifwata huku

(wao)*4 wajuaju wa kusema (vifuu tundu)
(wao)*4 wanasema yasomanaa (vijitu)
ndo maana hawapokewi kwasababu wana laana
(hapo saae*, hapa ndo kucha*)*4
(uliyonayo....lina huu... thamani yako*) {sauti}

 kila mwenye chuki na mie
[ujumbe huu umfikie       ]*2
mtazidi kunichukia na dunia mtaiona moto
(kindumbwendumbwe)*4
(wanalia)*3 wao!
(kumbe ni choyo)*3 wao!
(enh unashangaa mimi kula kwa mama ntilie, watu tumeshakula maholu*
sasa we ushamba wako hehe ee unataka nile kwa bi mkubwa wako? lakini hajui kupika, tena poole)

[mashaytwani yamepanda, yamekuja na mapanga]*2
[hata ukienda kwa mganga, na mizimu itaganda]*2
ukijipendekeza nakufyeka ooo
ukijipendekeza nakukata aaa nakukata
ukijipendekeza nakufyeka nakufyeka
ukijipendekeza nakukata aaa nakukata

(mashaytwani yamepanda)*2
mwalimu hafeli mtihani eeh kwa sababu yeye ndo anayeuandika
wakali wa hizi kazi, wakali wa hizi kazi wakali wa mashuzi
aaa poleni tena poleni saana
eee msitie huruma eh mara mmenuna nyie ee
shauri zao ee unauonja moto kwa ulimi
acha ukuunguze sasa

habari yako bwana Al hodari, salama tu
swalama, eee swalama
aaa nilikuwa nataka nikuulize kidogo, ehee uliza
hivi... wale rafiki zako mashoga?
eee wale mashoga mbona kitambo
unawajualakini nani na nani?
Anti muna Dachichi*.
haswaa
wale mashoga eti
halaa
ee zamani
haya basi waambie chei chei

mkinijibu tu, bwana wenu
na mkinyamaza, mnaniogopa
(mjibuni basi bwana wenu au ndo mnaniogopa, mnajua kuchumu lakini mnanuka midomo) {sauti}

Post a Comment

1 Comments

  1. This post inanikumbusha zile enzi shule ya upili wakati wa ushairi hehehe... I was going black those days, LOL, anyways thanks for this one Amigo

    ReplyDelete