Heshima Uongozini



 



Ndugu waheshimiwa, jiheshimuni, waheshimuni na wengine ili muheshimike kihalali!
Nanyi ‘msioheshimiwa’ muwaheshimu wenzenu na mamlaka zilizowekwa, jiheshimuni pia ndipo mdai heshima.

Kipindi kile nilipokuwa mdogo, mwalimu wangu Bi. Ong’uti Florence alipata kutujenga kwa hekima za waswahili. Si misemo, si wosia, si methali. Nakumbuka akitamka, ‘Heshima Si Utumwa.’
Taifa la Kenya limebadili huu msemo wa jadi. Kwetu sisi heshima ni utumwa, hivyo asikuambie mtu, lolote zaidi ya hayo.

Wenzangu ‘katika utumwa wa heshima,’ nakumbuka kioja alichokinasa Mwanahabari Larry Madowo barabarani kilichomhusu mheshimiwa aliyekuwa akivunja sheria barabarani bila haya. Huyo mheshimiwa hakutaka kuyavua magwanda yake ya heshima akawa mtumwa! Mtumwa wa kuzingatia sheria hadharani.

Wapo ‘watumwa’ wenye kulitakia nchi ufanisi, na kwa upande mwingine wapo ‘waheshimiwa’ wanaokereka sana na juhudi za amani na uwekezaji nchini.

Heshima, Kenya, ni sawa na ukoma, kila mwenye ishara hutengwa.

Hivi kumbuka kisa cha ‘mheshimiwa’ aliyefumaniwa na jenereta yenye thamani kubwa, iliyokusudiwa matumizi katika kaunti ya Tharaka Nithi katika mgahawa anayomiliki. Huu si utovu wa heshima kwa mali ya umma? Cha ajabu ni kwamba aliposwalishwa kwa mujibu wa fumanizi lile, alijitetea kwamba aliiomba akiwa afisini kama gavana na eti atairejesha tu.

Tena tusifanye wepesi katika kusahau yaliyojiri baina ya mwanahabari wa shirika la Nation Media (Justus Wanga) na msemaji katika afisi ya Naibu wa rais (David Mugonyi). Sauti yake msemaji huyu inarekodiwa  katika mazungumzo ya simu ikimtisha mwanahabari wa Nation. Chimbuko la tishio hili linaaminiwa kutokana na makala yaliyochapishwa katika gazeti la Sunday Nation lenye mada Cabinet seats that split Uhuru, Ruto.

Post a Comment

3 Comments

  1. Kazi nzuri sana aisee! Inapendeza kujua kuwa wapo wanaoenzi na kulivalia njuga hili suala la heshima katika jamii. Pongezi kwa kulipa kipao mbele hili jambo. Kazi njema!

    ReplyDelete